
|
Msimbo
|
Suluhisho
|
|
E-1
|
Hakikisha kwamba kebo ya Ethaneti imeunganishwa vizuri kwenye printa yako na kwenye kitovu au kifaa kingine cha mtandao.
Hakikisha kwamba kitovu au kifaa kingine cha mtandao kimewashwa.
Ikiwa unataka kuunganisha printa kwa kutumia Wi-Fi, weka tena mipangilio ya Wi-Fi ya printa kwa kuwa kimelemazwa.
|
|
E-2
E-3
E-7
|
Hakikisha kipanga njia chako cha pasi waya kimewashwa.
Thibitisha kwamba kompyuta au kifaa chako kimeunganishwa vizuri kwenye kipanga njia cha pasi waya.
Zima kipanga njia cha pasi waya. Subiri takriban sekunde 10, na kisha ukiwashe.
Weka printa karibu na kipanga njia chako cha pasi waya na uondoe vitu vyovyote kati yake.
Ikiwa umeingiza SSID kwa mikono, ikague ikiwa na sahihi. Angalia SSID kutoka kwenye sehemu ya Network Status kwenye ripoti ya muunganisho wa mtandao.
Ikiwa kipanga njia cha pasi waya kina SSID kadhaa, chagua SSID ambayo imeonyeshwa. Wakati SSID inatumia masafa yasiyotangamana, printa haizionyeshi.
Ikiwa unatumia usanidi wa kitufe cha msukumo kuanzisha muunganisho wa mtandao, hakikisha kipanga njia chako cha pasi waya kinakubali WPS. Huwezi kutumia usanidi wa kitufe cha msukumo ikiwa kipanga njia chako cha pasi waya hakikubali WPS.
Hakikisha SSID yako hutumia vibambo vya ASCII pekee (vibambo vya herufi na nambari na alama). Printa haiwezi kuonyesha SSID ambayo ina vibambo visivyokuwa vya ASCII.
Hakikisha unajua SSID na nenosiri lako kabla ya kuunganisha kwenye kipanga njia cha pasi waya. Ikiwa unatumia kipanga njia cha pasi waya na mipangilio yake msingi, SSID na nenosiri ziko kwenye lebo kwenye kipanga njia cha pasi waya. Ikiwa hujui SSID na nenosiri lako, wasiliana na mtu aliyekuwekea kipanga njia cha pasi waya, au ungalie hati zilizokuja pamoja na kipanga njia cha pasi waya.
Ikiwa unaunganisha kwenye SSID iliyotengenezwa kwa kutumia kipengele cha ufungaji cha kifaa maizi, kagua SSID na nenosiri kwenye hati zilizokuja pamoja na kifaa maizi.
Ikiwa muunganisho wako wa Wi-Fi utatenganishwa kwa ghafla, kagua hali zifuatazo. Ikiwa hali zozote kati ya hizi zinatumika, weka mipangilio ya mtandao wako upya kwa kupakua na kuendesha programu kutoka kwenye tovuti ifuatayo.
http://epson.sn > Mpangilio
Kifaa kingine mahiri kiliongezwa kwenye mtandao kwa kutumia usanidi wa kitufe cha uwasilishi.
Mtandao wa Wi-Fi ulisanidiwa kwa kutumia mbinu yoyote mbali na usanidi wa kitufe cha uwasilishi.
|
|
E-5
|
Hakikisha aina ya usalama ya kipanga njia cha pasi waya imewekwa kwa moja ya zifuatazo. Kama sivyo, badilisha aina ya usalama kwenye kipanga njia cha pasi waya, na kisha uweke upya mipangilio ya mtandao wa printa.
WEP-64 bit (40 bit)
WEP-128 bit (104 bit)
WPA PSK (TKIP/AES)*
WPA2 PSK (TKIP/AES)*
WPA (TKIP/AES)
WPA2 (TKIP/AES)
* WPA PSK pia inajulikana kama WPA Binafsi. WPA2 PSK inajulikana pia kama WPA2 Binafsi.
|
|
E-6
|
Kagua kama uchujaji wa anwani ya MAC umelemazwa. Ikiwa imewezesha, sajili anwani ya MAC ya printa ili isichujwe. Angali waraka uliotolewa pamoja na kipanga njia cha pasi waya kwa maelezo. Unaweza kukagua anwani ya kichapishaji ya MAC kutoka sehemu ya Network Status kuhusu ripoti ya muunganisho wa mtandao.
Ikiwa kipanga njia chako cha pasi waya kinashiriki uhalalishaji wa kushiriki na usalama wa WEP, hakikisha ufunguo na kiolezo cha uhalalishaji ni sahihi.
Ikiwa idadi ya vifaa vilivyounganishwa kwenye kipanga njia cha pasi waya ni chini ya idadi ya vifaa vya mtandao ambavyo unataka kuunganisha, fanya mipangilio kwenye kipanga njia cha pasi waya iongeze idadi ya vifaa vinavyoweza kuunganishwa. Angali waraka uliotolewa pamoja na kipanga njia cha pasi waya ili kufanya mipangilio.
|
|
E-8
|
Wezesha DHCP kwenye eneo la ufikiaji wakati Anwani Iliyopatikana ya IP ya kichapishaji imewekwa kwa Otomatiki.
Ikiwa Anwani Iliyopatikana ya IP ya kichapishaji imewekwa kwa Kikuli, anwani ya IP unayoweka kikuli huwekwa mbali na masafa (kwa mfano: 0.0.0.0). Weka anwani halali ya IP kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishaji au Web Config.
|
|
E-9
|
Kagua zifuatazo.
Vifaa vimewashwa.
Unaweza kufikia Intaneti na kompyuta nyingine au vifaa vya mtandao kwenye mtandao sawa kutoka kwa vifaa unavyotaka kuunganisha kwenye printa.
Ikiwa bado haiunganishi printa yako na vifaa vya mtandao baada ya kuthibitisha yaliyo hapa juu, zima kipanga njia cha pasi waya. Subiri takriban sekunde 10, na kisha ukiwashe. Weka upya mipangilio ya mtandao wako kwa kupakua na kuendesha kisakinishaji kutoka kwenye tovuti ifuatayo.
http://epson.sn > Mpangilio
|
|
E-10
|
Kagua zifuatazo.
Vifaa vingine kwenye mtandao vimewashwa.
Anwani za mtandao (anwani ya IP, anwani fiche, na njia changuo-msingi) ni sahihi iwapo umeweka Anwani ya Kupata IP kuwa Kikuli.
Weka upya anwani ya mtandao ikiwa hizo si sahihi. Unaweza kukagua anwani ya IP, anwani fiche, na njia msingi kutoka kwenye sehemu ya Network Status kwenye ripoti ya muunganisho wa mtandao.
Ikiwa DHCP imewezeshwa, badilisha Anwani Iliyopatikana ya IP ya kichapishaji kwa Otomatiki. Ikiwa unataka kuweka anwani ya IP kikuli, kagua anwani ya IP ya kichapishaji chako kutoka kwenye sehemu ya Network Status kwenye ripoti ya muunganisho wa mtandao, na kisha uteue Kikuli kwenye skrini ya mipangilio ya mtandao. Weka anwani fiche kwa [255.255.255.0].
Ikiwa bado haiunganishi printa yako na vifaa vya mtandao, zima kipanga njia cha pasi waya. Subiri takriban sekunde 10, na kisha ukiwashe.
|
|
E-11
|
Kagua zifuatazo.
Anwani ya njia msingi ni sahihi ukiweka mpangilio wa Usanidi wa TCP/IP wa Kichapishaji kwa Kikuli.
Kifaa ambacho kimewekwa kama njia msingi kimewashwa.
Weka anwani sahihi ya njia msingi. Unaweza kukagua anwani msingi kutoka kwenye sehemu ya Network Status kuhusu ripoti ya muunganisho wa mtandao.
|
|
E-12
|
Kagua zifuatazo.
Vifaa vingine kwenye mtandao vimewashwa.
Anwani za mtandao (Anwani ya IP, anwani fiche, na njia msingi) ni sahihi ikiwa unaziingiza kwa mkono.
Anwani za mtandao za vifaa vingine (anwani fiche na njia msingi) ni sawa.
Anwani ya IP haizozani na vifaa vingine.
Ikiwa bado haiunganishi printa yako na vifaa vya mtandao baada ya kuthibitisha yaliyo hapa juu, jaribu zifuatazo.
Zima kipanga njia cha pasi waya. Subiri takriban sekunde 10, na kisha ukiwashe.
Weka mipangilio ya mtandao tena kwa kutumia kisakinishaji. Unaweza kuiendesha kutoka kwenye tovuti ifuatayo.
http://epson.sn > Mpangilio
Unaweza kusajili manenosiri kadhaa kwenye kipanga njia cha pasi waya ambacho hutumia usalama wa aina ya WEP. Ikiwa manenosiri kadhaa yamesajiliwa, kagua kwanza kama nenosiri lililosajiliwa limewekwa kwenye printa.
|
|
E-13
|
Kagua zifuatazo.
Vifaa vya mtandao kama vile kipanga njia cha pasi waya, kitovu, na kipanga njia zimewashwa.
Usanidi wa TCP/IP wa vifaa vya mtandao vimesanidiwa kikuli. (Ikiwa Usanidi wa TCP/IP wa printa umewekwa kiotomatiki wakati Usanidi wa TCP/IP wa vifaa vingine vya mtandao vimetekelezwa kwa mikono, huenda mtandao wa printa ukatofautiana na mtandao wa vifaa vingine.)
Ikiwa bado inazozana baada ya kuangalia hii, jaribu ifuatayo.
Zima kipanga njia cha pasi waya. Subiri takriban sekunde 10, na kisha ukiwashe.
Weka mipangilio ya mtandao kwenye kompyuta ambayo iko kwenye mtandao sawa na printa kwa kutumia kisakinishaji. Unaweza kuiendesha kutoka kwenye tovuti ifuatayo.
http://epson.sn > Mpangilio
Unaweza kusajili manenosiri kadhaa kwenye kipanga njia cha pasi waya ambacho hutumia usalama wa aina ya WEP. Ikiwa manenosiri kadhaa yamesajiliwa, kagua kwanza kama nenosiri lililosajiliwa limewekwa kwenye printa.
|
|
Ujumbe
|
Suluhisho
|
|
*Multiple network names (SSID) that match your entered network name (SSID)
have been detected. Confirm network name (SSID).
|
Huenda SSID ile moja ikawekwa kwenye kipanga njia mbalimbali cha pasiwaya. Kagua mipangilio kwenye kipanga njia cha pasi waya, na ubadilishe SSID.
|
|
The Wi-Fi environment needs to be improved.
Turn the wireless router off and then turn it on.
If the connection does not improve,
see the documentation for the wireless router.
|
Baada ya kusogeza printa karibu na kipanga njia cha pasi waya na kuondoa vizuizi vyovyote, zima kipanga njia cha pasi waya. Subiri takriban sekunde 10, na kisha ukiwashe. Ikiwa hado haiunganishi, angalia hati zilizokuja pamoja na kipanga njia cha pasi waya.
|
|
*No more devices can be connected.
Disconnect one of the connected devices if you want to add another one.
|
Kompyuta na vifaa mahiri ambavyo vinaweza kuunganishwa kwa pamoja huunganishwa kikamilifu katika muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi). Ili kuongeza kompyuta au kifaa kingine mahiri, tenganisha kwanza moja ya vifaa vilivyounganishwa.
|
|
The same SSID as Wi-Fi Direct exists in the environment.
Change the Wi-Fi Direct SSID if you cannot connect a smart device to the printer.
|
Fungua paneli dhibiti ya printa, nenda kwenye skrini ya Usanidi wa Wi-Fi Direct na uchague menyu ili ubadlishe mpangilio. Unaweza kubadilisha jina la mtandao linalofuata baada ya DIRECT-XX-. Ingiza ndani ya vibambo 32.
|